Je wajua Njia Ya Kutambua Memory Card FEKI na Nzima
Umekwisha
nunua memori kadi (SD Card) ya GB 4, 8 n.k kisha muda wa kuitumia unagundua ni
nusu ya ujazo huo uliokua umeandikwa kwenye kadi? Au data zinakuwa zinapotea
mara kwa mara…Basi ujue umenunua SD Card feki.
Wengi huwa wanajikuta wanatumia pesa zaidi wakijua wanapata
memori kadi ya ukubwa unaoonekana juu ya kadi hizo lakini mwisho wa siku ni
utapeli tuu.
Tunashukuru walioulizia juu ya jambo hili na leo tutakufundisha njia kadhaa za kuzitambua kama ni orijino au feki.
Tunashukuru walioulizia juu ya jambo hili na leo tutakufundisha njia kadhaa za kuzitambua kama ni orijino au feki.
> KABLA YA KUNUNUA
Fahamu
aina za Memori kadi (SD Card)
Kuna aina kuu tatu. Hapa cha muhimu kujua ni kuzifahamu hizi
alama zake,ukikuta memori kadi imeandikwa ina ukubwa wa GB 8 na huku
ukiiangalia haina alama ya familia hiyo basi utambue unanunua kimeo.
1. SDSC or SD
Hizi zina ukubwa wa hadi GB 4

2.
SDHC- Ukubwa wa GB 4 – GB 32

Fahamu tofauti za muonekano wa logo na majina yake, SDSC(SD),
SDHC na SDXC…pia kiasi cha ukubwa unaotegemewa kwa aina hiyo ya memori kadi.
Ukiona tu haviendani ujue unanunua bomu. Kuna viwanda vingi bubu
vinavyotengeneza memori kadi na kuiga majina ya makampuni makubwa lakini huwa
hizo logo wanaweka ovyo ovyo tuu.
>USHANUNUA NA HAUNA UHAKIKA
Kama
umeshainunua na unaona inasumbua sumbua na unataka kujipa uhakikisho wa ubora
wake basi fuata njia hizi. Moja ya kwenye kompyuta na nyingine ya
kwenye simu.
Kwenye Kompyuta
Kuhakikisha
kwenye kompyuta kuna programu kadhaa, leo nitazitaja mbili zaidi zinazoaminika.
Kuna H2testw na FakeFlashTest.
Kupitia programu hizi utaweza kufahamu ujazo wa ukweli ulio kwenye memori kadi
au ata USB Flash.
Hakikisha unazi’test’ mpya mara baada ya kununua ili
kujihakikishia na hivyo kuwahi kurudisha kama inawezekana. H2testw ndio maarufu
zaidi.

Kwenye Simu
Pakua
app moja inaitwa SD Insights.App ya SD
Insights ikitoa taarifa kuhusu kadi iliyowekwa kwenye simu
Weka memori kadi yako kwenye simu na fungua app ya SD Insights. Inatakiwa kukupa taarifa zote muhimu kuhusu memori kadi yako.
Weka memori kadi yako kwenye simu na fungua app ya SD Insights. Inatakiwa kukupa taarifa zote muhimu kuhusu memori kadi yako.
Kama ni orijino au feki basi utapata kujua. Utapata taarifa
sahihi za ujazo (storage) wake, kampuni iliyoitengeneza, tarehe ya kutengenezwa
na kama ni kimeo utafahamu pia.
Muhimu kujua!: Ni
kawaida memori kadi ya ukubwa flani, mfano GB 4, kuwa na kama GB 3.8 hivi
badala ya 4 kamili. Tunachoongelea hapa ni tofauti kubwa.
Je wewe ushawahi kuuziwa kimeo? Sasa
kupitia tuliyoyaeleza utaweza kuepukana na hadhaa hii ya kufanywa Zeze na wauza
bidhaa feki.

No comments